KIVU YA KUSINI : Jamii ya Banyamulenge yahesabu vifo ya raia zaidi ya 400 tangu april 2017.

Jamii ya wanyamulenge huko fizi

Ni raiya zaidi ya 400 ya jamii yawa nyaùulenge ndiwo wamefariki tangu april 2017 jimboni kivu ya kusini yaelezea tangazo ya jamii hilo inayo papshwa kwenye mitandao.

Walio fariki wame ripotiwa katika wilaya za Fizi, Uvira na Itombwe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika machafuko ya jamii na vita mbali mbali zinazo onekana kila mara huko.

« Washiriki wa jamii la wanyamulenge  wanaonyesha kuwa  watu kadhaa waliojeruhiwa ; vijiji 318 vimeteketezwa kwa moto , wanawake kadhaa kubakwa, shamba kadhaa ziliharibiwa, vichwa 267,661 vya ng’ombe vilivyopigwa, shule 147 na vituo vya afya 55 viliangamizwa kabisa. » yaongeza jamii ya Banyamulenge.

Jamii ya Banyamulenge inayoishi mjini Bukavu inapendekeza kuona serikali ya Kongo isimamie mashambulio ya kila siku dhidi ya Banyamulenge na kutoa msaada kwa maelfu ya watu waliohamishwa ambao wanaishi katika hali « mbaya » vile vile arudishe usalama katika vijiji vyao  ili kuwaruhusu wakimbizi waliohamishwa warudi majumbani mwao.

Redaction

Commentez cette publication (Compte Facebook requis)

Janvier Barhahiga

Fondateur de BKINFOS.NET, Janvier est journaliste depuis plusieurs années. Informer est pour lui un moyen de participer au développement de son pays.